Kuthubutu
Hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali, hapa tunazungumzia uwezo na utayari wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya uoga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara, mradi n.k, watu wanaogopa hasara, hawajui jinsi ya kuendesha mradi wenyewe. Ili mtu awe mjasiriamali ni lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha ili baadae liweze kuleta tija kwake na kwa jamii pia.
Kuwa na uwezo wa kuongoza
Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai uongozi ni karama ombayo mtu anazaliwa nayo au anapewa na Mungu, ni kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha kuongoza, lakini mtu anaweza kujifunza na akawa kiongozi mzuri. Katika ujasiriamali uongozi ni jambo muhimu sana, mjasiriamali lazima aweze kuogoza biashara yake au mradi wake vizuri. Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kusimamia wafanyakazi na kutumia mbinu za uongozi ili apate matunda kwa kile ambacho anafanya.
Kupenda kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu kikubwa hapa ni lazima mjasiriamali awe anaipenda kwa dhati shughuli anayoifanya hii itamsaidia kufanya kazi kwa moyo. Kama unapenda kazi unayo fanya basi kazi hiyo haitakuwa ngumu bali, bali utakuwa unafanya kitu ambacho kwako unakipenda na mwisho wa siku utafanya kazi kwa bidii na maarifa. Watu waliofanikiwa ni wachapakazi hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
Kwenda na wakati
Mjasiriamali lazima aende na wakati ili aweze kutambua mabadiliko mbalimbali yanayo jitokeza katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa nafasi mjasiriamali kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko huria, kwenda na wakati pia kunatoa fursa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na kusoma magazeti, kufanya utafiti na kuhudhuria katika semina mbalimbali zinazohusu ujasiriamali.
Uaminifu na ukweli
Hii nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,wateja wengi wanapenda mtu mwamifu na mkwali. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya uamifu na ukweli ili upate wateja wengi, lazima uwe mkweli katika bei zako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako.
Dhamira
Mtu yeyote naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa kutosha, kufanya kazi kwa bidii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhamira. Lengo au dhamira ni motisha tosha itakayokupa msukumo mpaka kufikia mafanikio. Dhamira ya kweli inahitajika kabla ya kuingia katika biashara au mradi fulani.
Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, mjasiriamali lazima awe na na nidhamu katika biashara yake, awe na nidhamu katika matumiza yake ya pesa na ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii. Nidhamu ni chanzo cha mafanikiao.
Umakini na uelevu
Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi waliyokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo, anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe muelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment