Thursday, 30 April 2015
Friday, 24 April 2015
Jinsi ya kupata mtaji
Nini maana ya mtaji?
Watu
wengi wanaufahamu "Mtaji" kwa lugha rahisi kama "Kianzio" cha
biashara. Ni kweli, kwa mfano mtaji wa mama Ntilie ni Maji, sufuria,
jiko, mkaa, mwiko, sahani, pamoja na fedha ya kununulia chakula kama
mchele, nyanya, maharage, chumvi n.k.
Sasa basi katika mtiririko wa mahitaji yaliyotajwa hapo, vyote vinahitaji pesa ili kuvipata.

- Kukopa toka Benki au Mashirika ya Mikopo
Unachotakiwa kuwaonesha benki ni kuwa unabishara yenye mpango mzuri na unaweza kurudisha fedha hiyo ikiwemo riba ambayo ni faida yao.
Unaweza ukaanza na kiasi kidogo tu kama Milioni 1-5 na ukiweza kurudisha kama inavyotakikana basi unakuwa umejenga uaminifu na hivyo kuwa rahisi unapoomba kwa mara nyingine.
Ukiwa katika kikundi klwabaadhi ya mashrikaya fedha ni rahisi zaidi kupata mkopo kuliko ukiwa peke yako.Ukiwa na mali kama ardhi,nyumba au hata gari unaongeza uwezekano wa kuaminika na kupewa mkopo.
2. Vikundi vya Kuweka na Kukopa na Vikoba
Vikundi vya kuweka na kukopa na vile vya kuchangiana kwa madhumuni ya kukusanya fedha nyingi ya kutosha kufanya jambo kubwa kwa mmoja wa wanakikundi ni jinsi mojawapo ya kutumia fedha za watu wengine kujiendeleza.
Tengeneza mpango wa biashara ambao una faida na chukua fedha katika kikundi chako ulichojisajili. Hakikisha bishara yako inaweza kurudisha fedha kwa wakati kulingana na masharti ya kikundi chenu.
3. Kukopa toka Kwa Ndugu na Marafiki
Ndugu zako au marafiki ni mojawapo ya sehemu ya kupata mkopo. Mara nyingi mikopo ya watu hawa haina masharti magumu sana,japo ni hatari kama utashindwa kurudishakama ilivyopangwa kwani utahatarisha uhusiano wako nao.
Wakati mmoja katika familia ni masikini au anakosa mtaji wa bishara kuna ndugu mwingine anafedha isiyotumika kukua na kuleta faida (Fedha iliyolala). Tafuta jinsi ya kushawishi fedha hii itumike kujizalisha na mazao ya mtaji huo uwafaidishe wote,wewe mkopaji na mwenye fedha.
Uaminifu ni kitu cha msingi sana katika kufanikisha hili. Ukiwa mtu unayeaminika ni rahisi kwa ndugu na marafiki kukuamini na fedha zao. Uaminifu ni mtaji mkubwa katika mchezo wa fedha.
Thursday, 23 April 2015
Kanuni za Ujasiriamali
Kuthubutu
Hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali, hapa tunazungumzia uwezo na utayari wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya uoga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara, mradi n.k, watu wanaogopa hasara, hawajui jinsi ya kuendesha mradi wenyewe. Ili mtu awe mjasiriamali ni lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha ili baadae liweze kuleta tija kwake na kwa jamii pia.
Kuwa na uwezo wa kuongoza
Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai uongozi ni karama ombayo mtu anazaliwa nayo au anapewa na Mungu, ni kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha kuongoza, lakini mtu anaweza kujifunza na akawa kiongozi mzuri. Katika ujasiriamali uongozi ni jambo muhimu sana, mjasiriamali lazima aweze kuogoza biashara yake au mradi wake vizuri. Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kusimamia wafanyakazi na kutumia mbinu za uongozi ili apate matunda kwa kile ambacho anafanya.
Kupenda kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu kikubwa hapa ni lazima mjasiriamali awe anaipenda kwa dhati shughuli anayoifanya hii itamsaidia kufanya kazi kwa moyo. Kama unapenda kazi unayo fanya basi kazi hiyo haitakuwa ngumu bali, bali utakuwa unafanya kitu ambacho kwako unakipenda na mwisho wa siku utafanya kazi kwa bidii na maarifa. Watu waliofanikiwa ni wachapakazi hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
Kwenda na wakati
Mjasiriamali lazima aende na wakati ili aweze kutambua mabadiliko mbalimbali yanayo jitokeza katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa nafasi mjasiriamali kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko huria, kwenda na wakati pia kunatoa fursa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na kusoma magazeti, kufanya utafiti na kuhudhuria katika semina mbalimbali zinazohusu ujasiriamali.
Uaminifu na ukweli
Hii nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,wateja wengi wanapenda mtu mwamifu na mkwali. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya uamifu na ukweli ili upate wateja wengi, lazima uwe mkweli katika bei zako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako.
Dhamira
Mtu yeyote naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa kutosha, kufanya kazi kwa bidii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhamira. Lengo au dhamira ni motisha tosha itakayokupa msukumo mpaka kufikia mafanikio. Dhamira ya kweli inahitajika kabla ya kuingia katika biashara au mradi fulani.
Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, mjasiriamali lazima awe na na nidhamu katika biashara yake, awe na nidhamu katika matumiza yake ya pesa na ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii. Nidhamu ni chanzo cha mafanikiao.
Umakini na uelevu
Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi waliyokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo, anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe muelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
Maana ya Ujasiriamali
Dhana ya Ujasiriamali ina maana pana , miongoni mwa hizo ni;
Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya
katika hali yake ya kiuchumi ambaye ana tabia za kipekee ili
kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri) ili awe
na hali nzuri zaidi kiuchumi.
Ujasiriamali ni kitendo cha kuwa na tabia ya "Uthubutu". Hii tunaweza kuufananisha na uwezo (fursa) wa kutafuta masoko na kubuni vyanzo vipya vya biashara (Opportunities) ili mradi kuweza kuzalisha mali ama kutoa huduma itakayopelekea kuongeza kipato.
Ni mtafutaji Jasiri, anayethubutu kuamua kufanya biashara, mwenye uwezo wa kutambua mapema fursa mbalimbali za biashara, kukabiliana na vikwazo, na kutengeneza faida ya biashara hiyo.
Ujasiriamali ni sawa na usanii ambao ni lazima uingie ucheze sehemu yako mwenyewe. Mara nyingi bila kuwapo usimamizi wa biashara na uwepo wako unaweza kupoteza mwelekeo.
Pia katika hali nyingine
Mjasiriamali anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anajishughulisha
mwenyewe(amejiajiri) katika sekta fulani mfano: kilimo, ufugaji au
biashara.
Ujasiriamali ni kitendo cha kuwa na tabia ya "Uthubutu". Hii tunaweza kuufananisha na uwezo (fursa) wa kutafuta masoko na kubuni vyanzo vipya vya biashara (Opportunities) ili mradi kuweza kuzalisha mali ama kutoa huduma itakayopelekea kuongeza kipato.
Hata
hivyo yote haya yanahitaji muda, fedha na juhudi binafsi (Hii ni sawa
na ile dhana inayojulikana kama: "Mtaji wa masikini ni nguvu zake
mwenyewe").
Sifa za Mjasiariamali
Ni mtafutaji Jasiri, anayethubutu kuamua kufanya biashara, mwenye uwezo wa kutambua mapema fursa mbalimbali za biashara, kukabiliana na vikwazo, na kutengeneza faida ya biashara hiyo.
Ujasiriamali ni sawa na usanii ambao ni lazima uingie ucheze sehemu yako mwenyewe. Mara nyingi bila kuwapo usimamizi wa biashara na uwepo wako unaweza kupoteza mwelekeo.
Subscribe to:
Posts (Atom)